Meli ya Marekani yazingira maharamia

Meli ya kivita ya Marekani imefanya mawasiliano na meli ya Ukraine iliyokamatwa na maharamia wa kisomali wiki iliyopita ambayo ilitia nanga karibu na bandari ya Dobyo. ishara zaonyesha kuwa meli hiyo ya Marekani ya USS Howard inaikaribia meli ya MV Faina iliyobeba vifaru vya kivita 33 aina ya T-72. Meli hiyo ya MV Faina ilikuwa ikileta zana hizo humu nchini. Maharamia hao wameripotiwa kudai fidia ya dola za kimarekani milioni 35 lakini sasa wamepunguza kiwango hicho hadi kufikia dola ishirini za marekani ili kuiachia huru meli hiyo ya Ukraine na mabaharia wake. Hata hivyo, serikali ya Kenya imeonyesha wasiwasi juu ya ripoti hiyo ikisema kuwa hakukuwepo na taarifa za kutaka kulipwa fidia. Maharamia hao pia walitoa onyo dhidi ya jitihada zozote za kuokoa mabaharia na meli hiyo.

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph