Maharamia wa Kisomali wafyatuliana risasi.
Kumekua na ufyatulianaji wa risasi kati ya maharamia wa kisomali kwenye meli iliyotekwa nyara ikiwa na silaha. Afisa wa muungano wa wasafiri wa maji eneo la Afrika mashariki Andrew Mwangura amesema kuwa wanaume watatu walipigwa risasi kufuatia kutofautiana kuhusu mbinu ya oparesheni yao. Maharamia waliiandama meli ya Ukraine wiki iliopita na wameitisha dola milioni ishirini ili kuiachilia. Bwana Mwangura aliongeza kua hali hio ni mbaya huku meli ya MV Faina ikiwa imezingirwa na vyombo vya kijeshi vya Marekani. Kufikia sasa, maharamia hao wamekana madai ya ufyatulianaji risasi wakisema kuwa hakuna yeyote aliyepigwa risasi.