Mkutano wa IGAD kujadili usalama nchini Somalia waanza leo Nairobi
Mkutano wa siku mbili wa wanachama wa shirika la maendeleo la kimataifa wa nchi za Africa Mashariki na pembe ya Africa-IGAD ulianza hii leo jijini Nairobi. Baadhi ya wanachama wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na maafisa wakuu wa serikali ya mpito nchini Somalia huku mkutano huo ukujadili kwa kina visa vya uharamia katika pwani ya Somalia. Viongozi hao pia wanatafuta njia ya kusitisha mapigano kati ya makundi hasimu nchini Somalia. Msemaji wa shirika la IGAD Brasil Musumba amesema kuwa agenda kuu ya mkutano huo wa siku mbili ni amani na usalama nchini Somalia. Mkutano huo unaofanyika katika jumba la KICC unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbali mbali pamoja na wanachama wa shirika la IGAD.