Warsha ya kupanga kimbele katika wizara ya afya
Wizara ya afya na mipango kupitia shirika la Capacity project Kenya, linaandaa warsha ya siku tatu katika hoteli moja mjini Eldoret,ili kuwahamasisha maofisa wa afya wilayani umuhimu wa kupanga kimbele, ili kuwezesha wizara ya afya kuchangia kuafikia riwaza ya mwaka alfu mbili na thelathini.Kulingana na afisa wa wilaya ya huduma za afya Ben Osire,kupanga kimbele kuanzia wilayani husaidia kuzingatia na kutambua mahitaji muhimu kwa sababu ya rasilimali chache ambazo hupatikana.
Osire alisema kupanga kimbele ni muhimu, lakini kwa miaka nenda miaka rudi imepuuziliwa na kupelekea kudorora kwa huduma inazotoa wizara ya afya kwa umma zikiwemo sababu zingine.Osire alifichua kuwa ili kuafikia riwaza ya alfu mbili na thelathini,ni lazima kwanza kuhakikisha kuwa tuna taifa lenye afya.
Mwisho…….jimmy kitiro