Jeshi la Kenya na lile la Marekani washirikiana kujenga shule katika mkoa wa bonde la ufa
Jeshi la Kenya likishirikiana na jeshi la Marekani linajenga shule zilizoharibiwa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi katika mkoa wa bonde la ufa.Shughuli hizo za ujenzi zimekuwa zikiendelea katika maeneo kadhaa katika mkoa huo chini ya mpango wa “Oparesheni Jenga Mashule”.Majeshi hao wanafanya ukarabati wa shule 19 katika mkoa wa bonde la ufa. Katika wilaya ya Molo wanakarabati shule 16 huku katika wilaya ya Transnzoia wanakarabati shule 3.Shughuli hiyo ya ukarabati imegarimu zaidi ya shilingi milioni 280 chini ya mpango wa “Oparesheni Jenga Mashule” ya jeshi la Kenya na “Quick Impact Project” ya jeshi la Marekani.Waliohudhuria shughuli hiyo ya kuanzishwa kwa ujenzi ni pamoja na askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Eldoret Cornelius Korir, shirika la haki na amani la kanisa katoliki, mashirika yasiyo ya kiserikali baadhi ya mashirika mengine.