ODM kutoa msimao kuhusu ripoti ya Waki
Wabunge kutoka chama cha ODM wanakutana hii leo huku agenda kuhusu mjadala wa ripoti ya Waki ukitarajiwa kupewa kipaumbele katika mkutano huo. Wabunge wa chama hicho wanataka kufanyika kwa mjadala ili kuwawezesha kutoa msimamo wa pamoja kama chama kuhusiana na swala hilo ambalo limezua hisia tofauti katika chama hicho. Waziri mkuu Raila Odinga na naibu wake Musalia Mudavadi wameunga mkono kutekelezwa kwa mapendekezo ya ripoti hiyo huku waziri wa kilimo William Rutoh na mwenyekiti wa chama hicho Henry Koskei wakitupilia mbali ripoti hiyo. Wakati uo huo, waziri wa ustawishaji wa maeneo Fred Gumo amezungumzia swala hilo na kusema ikiwa utekelezaji wa ripoti hiyo utawagawanya wakenya, basi hapana haja ya kutekeleza mapendekezo hayo na badala yake amewataka wakenya kusameheana, kusahau yaliyopita na kuangazia maendeleo.