Sasa Kalonzo auipinga ripoti ya Waki
Makamu wa rais Kalonzo Musyoka sasa ameungana na viongozi wanaoupinga ripoti ya Waki.Kalonzo amesema kuwa mapendekezo ya ripoti hiyo kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi ambayo imezua hisia mbali mbali kutoka kwa viongozi haina ushahidi wa kutosha ya kumuhukumu yeyyote mahakamani.Makamu wa rais amedokeza kuwa baraza la mawaziri litaafikiana kuhusu njia mwafaka utakaomaliza uhasama huo bila ya kuhitilafia shughuli ya uponjaji na maridhiano humu nchini bada ya ghasia hizo za baada ya uchaguzi.Aidha Kalonzo amesema kuwa kubuniwa kwa mahakama ya uhalifu wakivita kama ile iliyochunguza visa vya mauaji ya halaiki nchini Rwanda itakuwa tu ni kupoteza wakati akidokeza kuwa makama kama hayo kwa mara nyingi hukosa kupata ushahidi wa kutosha kutoa hukumu.