Serikali yajizatiti kupunguza bei ya mafuta nchini
Wakenya huenda wakawa na habari njema katika muda wa siku chache zijazo kuhusiana na kiasi cha pesa watakazotumia kununua mafuta. Hayo huenda yakajiri baada ya serikali kutangaza kuwa itachapisha bei ambazo kampuni za mafuta zitalazimika kuzingatia. Waziri wa kawi Kiraitu Murungi ameliamurisha shirika la mafuta nchini kuagiza kutoka nje asilimia thelathini ya mafuta yote yanayotumika humu nchini mbali na kufungua vituo themanini na sita zaidi vya mafuta. Waziri huyo aliambia bunge hiyo jana kuwa hatua hiyo itamlinda mwananchi wa kawaida dhidi ya bei ghali ya mafuta. Serikali imekuwa ikijaribu mbinu tofauti za kutaka kupunguzwa kwa bei ya bidhaa hiyo ambayo kufikia sasa haijafaulu.