Siku ya amani kwa shule yafanyika mjini Eldoret
Wanafunzi kutoka mji wa Eldoret hii leo walifanya matembezi ya amani katika barabara za mji huo katika harakati ya kuhubiri amani baina yao na jamii kwa jumla.Kwa mujibu wa mshirikishi wa shughuli hiyo kutoka kanisa katoliki dayosisi ya Eldoret chini ya idara ya elimu mtawa Cecilia Muthoni, kanisa katoliki liliona vyema kuandaa hafla yenye mada “tuungane mioyo katika juhudi za kuhubiri amani shuleni”kufuatia yale ambao wanafunzi waliyoyaona wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi. Katibu wa elimu katika kanisa hilo James murei,alisema kuwa kanisa katoliki linakusudia kuwaelimisha wanafunzi na jamii kuhusu umuhimu wa kuishi kwa amani akidokeza kuwa maendeleo hayawezi kufanyika ikiwa hakuna amani.
Mwisho……jimmy kitiro