Vijana wapewa changamoto kuendelea na masomo iwapo wanaazimia kujiunga na jeshi

Vijana wanaoazimia kujiunga na jeshi la Kenya hawana budi ila kufanya bidii shuleni ili kusajiliwa katika jeshi.Akizungumza katika eneo la Burnt Forest mjini Eldoret, Meja Chris Orina kutoka kitengo cha jeshi cha 12 engineers alisema kuwa jeshi halifai kutazamiwa kama kitengo cha kuwasukuma vijana ambao hawakufaulu mitihani yao ya kitaifa.Meja Orina alidokeza kuwa vijana ni sharti wasome hadi katika vyuo vya masomo ya hali ya juu na wafuzu ndiposa waweze kusajiliwa katika jeshi.Aliongeza kuwa shughuli kadhaa za ujenzi na ukarabati ambazo zinaendelea humu nchini zinafanywa na vijana ambao waliendelea na masomo na wakafuzu na hatimaye wakasajiliwa kama wanajeshi wenye ujuzi wa mambo tofauti.Meja Orina anasimamia ujenzi wa shule ambazo ziliharibiwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi katika mkoa wa bonde la ufa katika shughuli inayoitwa “Oparesheni Jenga Mashule”. Anashirikiana na wanajeshi kutoka Marekani chini ya mpango wa “Quick Impact Project”.

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph