Washukiwa wa uteketezaji wa kanisa Kiambaa wafikishwa katika eneo la mkasa

Watu wanne ambao wanashukiwa kuwauwa watu katika kanisa la KAG Kiambaa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi hii leo walifikishwa katika eneo la tukio hilo ambapo mahakama kuu ilizuru.Mamia ya watu walifika katika eneo hilo ambapo jaji David Maraga wa mahakama kuu ya Nakuru alisikiza ushahidi kutoka kwa mshahidi mmoja supritenant wa polisi Jonathan Ngala ambaye alifanya uchunguzi kuhusu kesi hiyo.Zaidi ya polisi 50 na walinzi wa magereza walikuwa wakishika doria katika kanisa hilo huku washukiwa hao wakifikishwa katika eneo la kisa hicho cha uteketezi chini ya ulinzi mkali.Supritenant Jonathan Ngala akitoa ushahidi wake alisema kuwa alifika kanisani mwendo wa saa tano unusu asubuhi na kupata kanisa hilo likiwa bado linateketea na akaweza kuhesabu miili 8 na mengine 5 katika mashamba yaliyoko karibu.Pia aliongeza kuwa aliupata mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye kiti cha gurudumu nje ya kanisa hilo.

Mwisho Kentis Onyatch

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph