Katiba mbaya yahitilafia shughuli za KACC
Shirika la kupambana na ufisadi nchini KACC limesema kuwa ilikuwa vigumu kwao kuwachunguza na kuwashtaki wanasiasa wakuu humu nchini kutokana na hali ya sasa ya katiba.Mwenyekiti wa shirika hilo jaji Aaron Ringera amesema kuwa kesi zilizowasilishwa mbele ya tume yake haziwezi kuchunguzwa vikamilifu maana zilifutiliwa mbali na baadhi ya wahusika kutokana na sheria mbaya.Kwa sasa jaji Ringera anapendekeza kujumuishwa kwa shirika la kupambana na ufisadi nchini kwenye katiba punde tu marekebisho ya katiba yatapokamilika ili kutoa nafasi kwao kutekeleza majukumu yao vikamilifu