Masai ahimiza kanisa liwajibike kuhusiana na ukimwi

Waumini na viongozi wa makanisa wana jukumu kusaidia taifa kukumbana na janga la Ukimiwi katika Wilaya ya Trans-Nzoia. Hayo yamesemwa na kiongozi wa Chama Cha Uzalendo katika eneo bunge la Cherangany, Bwana Jesse Masai, katika mashauri kuhusiana na janga hilo leo hii jijini Nairobi.Bwana Masai alisema Wakristo, katika sehemu hiyo yenye waumini wengi,wana jukumu la kuhakikisha raia wengi wanatambua hali yao, na pia
kupata tiba na lishe bora.Kiongozi huyo alisema serikali haitaweza kukimu mahitaji yote yawahasiriwa wa virusi hivyo hatari, na kuongeza kuwa kanisa lina nafasikubwa zaidi kubadilisha maisha hadi tiba kamilifu takapopatikana.
Wakati uo huo, Bwana Masai amekashifu viongozi wa kisiasa kutoka mkoa
wa Bonde la Ufa wanaoaminika kuhusika na sakata ya ukosefu wa unga wa
mahindi nchini, na kuongeza kuwa itakuwa aibu iwapo wakazi wa eneo hilo
wataumia kwa njaa sasa au mwaka ujao kutokana na ulafi huo.

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph