Wakulima wataka mahindi kununuliwa kwa shilingi 2360
Wakulima kutoka eneo la North Rift wametishia kutouzia mahindi yao shirika la kitaifa la mazao na nafaka nchini hadi pale nafaka yao yatanunuliwa kwa bei watakayokubaliana nayo.Mkulima maarufu ambaye pia ni mkurugenzi wa shirika la ukuzaji nafaka Timothy Busienei akizungumza kwa niaba ya wakulima alisema kuwa wakulima wanataka shirika la kitaifa la mazao na nafaka nchini kununua mahindi yao kwa bei ya shilingi 2,360.Wakulima hao ambao walifanya mkutano hii leo katika uwanja wa michezo wa Kipkeino mjini Eldoret pia wameitaka serikali kufufua shirika la wakulima nchini la KFA ili kuwawezesha kupata bidhaa za matumizi shambani kwa bei ya chini.Wakulima hao sasa wameipa wizara ya kilimo hadi wiki ijayo kuangazia swala hilo la sivyo watakoma kupeleka nafaka yao katika halmashauri hiyo nafaka nchini.Serikali ilitangaza siku ya Jumatatu kuwa itaagiza mahindi kutoka nchi ya nje na kuiuzia viwanda vya kusaga unga kwa bei shilingi 1950, bei ambayo wakulima wameikataa.