Mkutano wa Geneva wafikiwa kikomo chake hii leo

Mkutano ulioitishwa na mpatanishi mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu humu nchini Dakta Koffi Annan jijini Geneva ulifikia kikomo chake hii leo.Akitoa hotuba yake ya mwisho wakati wa kufunga rasmi  mkutano huo hii leo, Annan alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na kusudi la kupata mafunzo yatakayotumika kusuluhisha mizozo sawia na hiyo itakapotokea katika mataifa mengine.Annan aliwaomba viongozi humu nchini kuwajibika vilivyo na kutekeleza mipango ya marekebisho kama ilivyopitishwa katika mkataba huo wa mapatano.Mpatanishi huyo vile vile, amewataka wananchi  kuwajibika kwa kuwashinikiza viongozi kutekeleza agenda ya mabadiliko.Akizungumza katika hafla hiyo, naibu waziri mkuu Musalia Mudavadi ambaye aliongoza ujumbe wa Kenya katika mkutano huo aliishukuru wakfu wa Koffi Annan kwa kuunga mkono serikali ya muungano katika kutekeleza mipango yake kama ilivyoafikiwa katika mkataba wa amani

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph