Ahmed Hassan ateuliwa kuongoza tume huru ya uchaguzi nchini
Ahmed Issak Hassan ameteuliwa kuchukua wadhifa wa uenyekiti wa tume huru ya mpito ya uchaguzi nchini-IICC.Hapo awali Hassan aliwahi kuhudumu kama mwanachama wa tume ya marekebisho ya katiba nchini.Akizungumza hii leo muda mfupi baada ya uteuzi huo kutangazwa na kamati teule ya bunge iliyotwika majukumu ya marekebisho ya katiba, Hassan alisema kuwa kamwe hatowaaibisha wakenya na kuwa yuko tayari kwa kazi hiyo ikiwa bunge litamuidhinisha kuongoza tume hiyo ya uchaguzi.Hassan mweye umri wa miaka thelathini na tisa amefanya kazi ya sheria ytangu mwaka wa 1995 na kwa sasa anahudumu kama wakili wa mahakama kuu.Wakenya wengine waliokuwa wakiwania wadhifa huo ni pamoja na aliyekuwa spika wa bunge Francis Ole Kaparo, aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu Maina Kiai na Koki Muli ambaye alikuwa meneja mkurugenzi wa taasisi ya elimu na democrasia.
Mwisho…Chumba Silvanoh