Kanoute atia sahihi kandarasi mpya na klabu ya Sevilla
Mshambulizi wa timu ya taifa ya Mali Frederic Kanoute amekubali kuongeza muda wa kandarasi yake na klabu anayechezea ya Uispania ya Sevilla.Hatua hiyo sasa itamweka kwenye klabu hiyo hadi mwaka wa 2012 kulingana na taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya klabu ya Sevilla. Mshambulizi huyo matata atakuwa ameitimisha miaka thelathini na nne kandarasi hiyo itakapofikia kikomo chake.Kanoute ndiye mchezaji mwenye mabao mengi msimu huu katika klabu hiyo akiwa ameandikisha mabao kumi na tano.Aliteuliwa mwanandinga bora barani Africa Africa wa CAF mwaka wa 2007.
Mwisho…Chumba Silvanoh