Mutua ataka wakenya kuzingatia usafi ili kuzuia maradhi ya kipindupindu

Msemaji wa serikali Dakta Alfred Mutua amewaomba wananchi kudumisha usafi wa hali ya juu ili kuzuia kusambaa kwa maradhi ya kipindupindu.Katika taarifa yake ya kila wiki kwa vyombo vya habari, Mutua alizitaka utawala za kimkoa kufunga vyumba vya kuuza vyakula ambavyo havizingatii hali ya usafi.Aidha amewataka wananchi kukumbatia mbinu za kujikinga ili kuepukana na maradhi hayo kama vile kunywa maji yaliyochemshwa na kuosha mikono kabla ya kula chakula na baada ya kutoka msalaani.Aidha amewaomba wananchi kutumia vyakula vilivyochemshwa vyema na kumwona daktari haraka iwezekenavyo punde tu anapohisi kuumwa na tumbo na kuanza kutapika.Matamshi ya msemaji wa serikali yanajiri huku hali ya tahadhari ikitolewa kufuatia mkurupuko wa maradhi ya kipindupindu katika maeneo mbali mbali nchini na kusababisha vifo zaidi ya watu arubaini kufikia sasa.

Leave a Reply

XHTML: You can use these tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>

:mrgreen: :neutral: :twisted: :shock: :smile: :???: :cool: :evil: :grin: :oops: :razz: :roll: :wink: :cry: :eek: :lol: :mad: :sad:

Isulong SEOph