Mbunge wa Garsen Danson Mungatana amejiuzulu kama waziri msaidizi katika wizara ya huduma za matibabu siku moja tu baada ya kiongozi wa chama chake Martha Karua kung’atuka serikalini vile vile.Akitangaza uamuzi huo, Mungatana ambaye ni katibu mkuu wa chama cha Narc Kenya aliitaka serikali kuwajibika vilivyo na kuzingatia kwa makini maswala ya marekebisho.Uamuzi huo wa Mungatana unajiri saa chache tu baada ya mkutano wa wabunge wa chama cha Nark Kenya uliofanyika mapema hii leo.Wakati wa mkutano huo, Chama cha Nark Kenya kilisema kuwa kinaheshimu uamuzi wa kiongozi wake wa kugura serikali na kuafikiana kuwa wanachama wengine wa chama hicho walio serikalini wana huru wa kusalia serikalini bila ya kushurutishwa.
This entry was posted
on Tuesday, April 7th, 2009 at 10:45 am and is filed under Fahamu Ya Fish.
You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0 feed.
You can skip to the end and leave a response. Pinging is currently not allowed.