Serikali yatakiwa kutoa hati umiliki shamba kwa shule zilizo katika ardhi ya misitu
Chama cha muungano wa wazazi nchini kimeitaka serikali kutoa hati ya umiliki shamba kwa shule zilizo katika ardhi iliyotengewa misitu.Katibu mkuu wa chama hicho Musau Ndunda amefichua kuwa shule 175 wilayani Marakwet zimejengwa katika ardhi ya misiti na hazina hati ya umiliki wa shamba hizo.Wakati uo huo, Ndunda amedokeza kuwa hali ya elimu nchini imezidi kudorora kufuatia kubadilishwa kwa taasisi za kiufundi kuwa bewa wa vyuo vikuu na hivyo kutoa wasomi badala ya wataalamu.Akitoa mfano wa taasisi ya Kenya Science ambayo imechukuliwa na chuo kikuu cha Kenyatta, Ndunda alimsihi waziri wa elimu ya juu Sally Kosgei kuingilia kati na kuhakikisha kuwa sera mwafaka ya elimu inabuniwa humu nchini ili kuhifadhi kiwango cha juu cha elimu na utaalamu.Katibu huyo mkuu wa chama cha wazazi alikuwa akizungumza katika warsha ya walimu na wazazi kutoka eneo la North Rift lililokuwa likiangazia changamoto zinazoikumba sekta ya elimu nchini kwa uhusiano na malengo ya 2030.
Mwisho…Carolyne koech