Mpango wa kazi kwa vijana wafika Eldoret,
Serikali kupitia baraza la manispaa la mji wa Eldoret imetoa nafasi za kazi kwa vijana wa mji huo. Meya wa mji wa Eldoret Samuel Rutoh amefichua kuwa serikali imetenga nafasi 1600 za ajira kupitia kwa mpango wa kazi kwa vijana utakaotekelezwa na baraza lake. Rutoh amedokeza kuwa kazi hizo zitawafanya vijana kuwa na shughuli na hivyo kuwaepusha kujihusisha na maovu. Alisema kuwa nafasi hizo za ajira ni kama vile uzoaji taka, ukarabati wa barabara na huduma ya kusafisha na kunadhifisha mji.
Aliongeza kuwa vijana watahitajika kuwa na vitambulisho vyao vya kitaifa na kadi ya kupigia kura ili kuweza kuajiriwa na hivyo kuwaomba madiwani kuwahamasisha vijana katika wadi zao kupata stakabadhi hizo muhimu.
Aidha meya Rutoh ameishukuru serikali pamoja na madiwani kwa kuungana ili kutoa nafasi hizo za ajira kwa vijana.
Mwisho…Emma Anyango