Watu kumi wapata majeraha baada ya kuhusika katika ajali
Ajali mbaya ya barabara iliyotokea mapema hii leo Asubuhi ambayo ilihusisha magari mawili karibu na hospitali ya Mediheal iliyokaribu na ikulu ndogo ya rais mjini Eldoret iliwaacha watu kumi kuuguza majeraha.
Kwa mujibu wa aliyeshuhudia ajali hiyo abiria waliokuwa kwenye viti vya mbele walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo. Wahisani wema walijitokeza baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kuwasaidia waliohusika kwa kuwapeleka katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret kupata matibabu.