Archive for the 'Fahamu Ya Fish' Category

Ajali mbaya ya barabara iliyotokea mapema hii leo Asubuhi ambayo ilihusisha magari mawili karibu na hospitali ya Mediheal iliyokaribu na ikulu ndogo ya rais mjini Eldoret iliwaacha watu kumi kuuguza majeraha.

Tuesday, May 5th, 2009

Wazazi wameshauriwa kuhakikisha kuwa watoto wao wanapata chanjo ya kuwazuia kutokana na magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa. Akizungumza hii leo katika afisi yake, afisa mkuu wa matibabu katika wilaya ya Eldoret Magharibi Daktari Bill Lubanga,alisema kuwa kampeini  inayoendelea ya malezi bora inanuia kuwahudumia watoto alfu mia moja na sabini (170,000) wenye umri wa chini ya miaka [...]

Watu kumi wapata majeraha baada ya kuhusika katika ajali

Tuesday, May 5th, 2009

Ajali mbaya ya barabara iliyotokea mapema hii leo Asubuhi ambayo ilihusisha magari mawili karibu na hospitali ya Mediheal iliyokaribu na ikulu ndogo ya rais mjini Eldoret iliwaacha watu kumi kuuguza majeraha.
Kwa mujibu wa aliyeshuhudia ajali hiyo abiria waliokuwa kwenye viti vya mbele walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo. Wahisani wema walijitokeza baada ya kutokea kwa ajali [...]

Maafisa wa polisi wanasa misokoto ya bangi.

Tuesday, May 5th, 2009

Watu wawili wanawasaidia polisi kufanya uchunguzi baada ya kunaswa na misokoto alfu 12 ya bangi. Maafisa wa Polisi walinasa bangi hiyo katika barabara kuu ya Mombasa kuelekea Nairobi na inaaminika bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kuelekea nchi jirani ya Tanzania kupitia Mombasa.
Bangi hiyo iliyokuwa ikisafirishwa kwa magari ya kibinafsi zilinaswa mahali tofauti tofauti. Misokoto alfu 10 [...]

Mpango wa kazi kwa vijana wafika Eldoret,

Tuesday, May 5th, 2009

Serikali kupitia baraza la manispaa la mji wa Eldoret imetoa nafasi za kazi kwa vijana wa mji huo. Meya wa mji wa Eldoret Samuel Rutoh amefichua kuwa serikali imetenga nafasi 1600 za ajira kupitia kwa mpango wa kazi kwa vijana utakaotekelezwa na baraza lake. Rutoh amedokeza kuwa kazi hizo zitawafanya vijana kuwa na shughuli  na [...]

Wakimbizi wa ndani wadai maafa yatokana na njaa

Tuesday, May 5th, 2009

Wakimbizi wa ndani kwa ndani walioweka makaazi katika kambi ya ukimbizi katika uwanja wa maonyesho ya kilimo mjini Eldoret wanadai kuwa maafa ambayo yametokea katika kambi hiyo katika siku za hivi maajuzi yametokana na njaa. Kwa mujibu wa afisa msimamizi katika kambi hiyo Mwangi Gikonyo, chakula walichopokea wiki iliyopita haitoshi kuwasukuma hadi muda wa wiki [...]

Waliotarajiwa kunufaika na bidhaa za ukulima walalamika

Tuesday, May 5th, 2009

Zaidi ya wakulima elfu tatu katika eneo la Turbo waliopangiwa kunufaika na pambajeo za bure za ukulima kutoka kwa serikali wameiomba serikali kuharakisha utoaji wa bidhaa hizo kabla ya msimu wa upanzi wa mahindi kuisha. Wakiongozwa na mwakilishi wao David Ngenda wakaazi hao ambao wengi wao ni waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wanadai [...]

Serikali yatakiwa kutoa hati umiliki shamba kwa shule zilizo katika ardhi ya misitu

Tuesday, April 7th, 2009

Chama cha muungano wa wazazi nchini kimeitaka serikali kutoa hati ya umiliki shamba kwa shule zilizo katika ardhi iliyotengewa misitu.Katibu mkuu wa chama hicho Musau Ndunda amefichua kuwa shule 175 wilayani Marakwet zimejengwa katika ardhi ya misiti na hazina hati ya umiliki wa shamba hizo.Wakati uo huo, Ndunda amedokeza kuwa hali ya elimu nchini imezidi [...]

PNU, ODM yafanya mikutano ya dharura

Tuesday, April 7th, 2009

Chama cha  PNU hii leo kilikita kambi katika jumba la KICC kujadili maswala mbali mbali yanayoikumba serikali ya muungano.Mkutano huo wa PNU uliongozwa na makamu wa rais Kalonzo Musyoka huku ajenda kuu ikiwa ni kujadili serikali ya muungano.Akizungumza baada ya mkutano huo, makamu wa rais Kalonzo Musyoka alitupilia mbali madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu Raila [...]

Maafisa wa Uganda wawanasa wavuvi wa Kenya katika kisiwa cha Migingo

Tuesday, April 7th, 2009

Maafisa wa usalama wa Uganda wamewatia nguvuni wakenya tisa katika kisiwa hicho cha migingo kwa madai ya kutekeleza shughuli zao za uvuvi katika maeneo yao.Hali ya taharuki imetanda katika kisiwa hicho ambacho kinazozaniwa na taifa la Kenya na Uganda huku kila mmoja akidai umiliki wa kisiwa hicho.Akidhibitisha kisa hicho, msemaji wa polisi Eric Kiraithe alisema [...]

Mungatana ang’atuka serikalini

Tuesday, April 7th, 2009

Mbunge wa Garsen Danson Mungatana amejiuzulu kama waziri msaidizi katika wizara ya huduma za matibabu siku moja tu baada ya kiongozi wa chama chake Martha Karua kung’atuka serikalini vile vile.Akitangaza uamuzi huo, Mungatana ambaye ni katibu mkuu wa chama cha Narc Kenya aliitaka serikali kuwajibika vilivyo na kuzingatia kwa makini maswala ya marekebisho.Uamuzi huo wa [...]