Archive for the 'Fahamu Ya Fish' Category

Bunge lina hadi mwezi Agosti kubuni mahakam maalum

Wednesday, April 1st, 2009

Aliyekuwa Katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mpatanishi mkuu katika mzozo wa kisiasa humu nchini daktari Koffi Annan amesema kuwa bunge la Kenya lina hadi tarehe thelathini na moja mwezi agosti mwaka huu kubuni mahakama maalum itakayosikiza kesi za washukiwa waliochochea ghasia za baada ya uchaguzi.Annan amesema ikiwa mahakama hiyo itakosa kubuniwa, bila shaka [...]

Meneja mpya wa halmashauri ya viwanja vya ndege nchini kutangazwa Ijumaa

Wednesday, April 1st, 2009

Kandarasi ya utenda kazi ya meneja mkurugenzi anayeondoka wa halmashauri ya viwanja vya ndege nchini George Muhoho hautaongezwa kulingana na waziri wa usafiri Chirau Ali Makwere.Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Makwere alifichua kuwa mkurugenzi mpya wa halmashauri hiyo atatangazwa siku ya ijumaa wiki hii.Haya yanajiri huku kukizuka madai ya kashfa ya kukodisha shamba [...]

Hali ya kawaida imerejea mjini Eldoret baada ya athari za ghasia za baada ya uchaguzi

Wednesday, April 1st, 2009

Hali ya kawaida katika mji wa Eldoret imerejelea hali yake ya kawaida baada ya kukumbwa pakubwa na ghasia za baada ya uchaguzi  mapema mwaka wa 2008.Afisa anayehusika na maswala ya maendeleo katika wilaya ya Eldoret Mahgaribi Martin Wekesa amewaelezea wafanyibiashara kuwa kuna nafasi bora ya kuwekeza mjini Eldoret na kuwahakikishia kuwepo kwa usalama wa kutosha.Wekesa [...]

Wanaharakati mjini Eldoret washurutisha wabunge kulipa ushuru

Wednesday, April 1st, 2009

Kituo cha kutetea haki za kibinadamu na demokrasia mjini Eldoret hii leo imezindua kampeini inayolenga kuwashurutisha wabunge kulipa ushuru mada yake ikiwa “ wabunge lazima walipe ushuru”.
Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Ken wafula amesema kuwa ni jambo la aibu kwa wabunge watatu pekee kulipa ushuru kati ya wabunge 222.
Wabunge hao wawili ni pamoja na Johnstone [...]

Rais wa Burundi awasili humu nchinikwa ziara yasiku tatu

Wednesday, April 1st, 2009

Rais wa Burundi Piekh Nkurunzinza amewasili humu nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu katika harakati ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya Kenya na Burundi.
Mataifa haya mawili yanatarajiwa kutia sahihi mikataba kadhaa ya kibiashara katika sekta mbali mbali wakati wa ziara hiyo.
Ndege iliyombeba rais huyo wa Burundi ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa [...]

Netanyahu aapishwa Waziri Mkuu Israel

Wednesday, April 1st, 2009

Bunge la Israel limemuapisha Benjamin Netanyahu kuwa Waziri Mkuu na limeidhinisha baraza jipya la mawaziri lenye muelekeo wa mrengo wa kuume kwa kura 69 dhidi ya 45. Netanyahu mapema alilitaka bunge la nchi hiyo kumuamini ili aiongoze Israel katika wakati huu wa mtikisiko wa uchumi pamoja na changamoto za kiusalama ambazo nchi hiyo zinakabiliana nazo. [...]

Obama ataka vitendo kuikwamua dunia

Wednesday, April 1st, 2009

Rais Barack Obama wa Marekani amesisitiza umuhimu wa kuwa na mwelekeo wa kasi katika kukabiliana na kudorora kwa uchumi duniani. Rais Obama amekutana na Gordon Brown katika afisi ya Waziri Mkuu ya Downing Street siku moja kabla ya viongozi wa dunia hawajakutana katika mkutano wa G20. Rais Obama pia amesema dunia inakabiliana na kipindi kigumu [...]

Mkutano wa Geneva wafikiwa kikomo chake hii leo

Tuesday, March 31st, 2009

Mkutano ulioitishwa na mpatanishi mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu humu nchini Dakta Koffi Annan jijini Geneva ulifikia kikomo chake hii leo.Akitoa hotuba yake ya mwisho wakati wa kufunga rasmi  mkutano huo hii leo, Annan alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na kusudi la kupata mafunzo yatakayotumika kusuluhisha mizozo sawia na hiyo itakapotokea katika [...]

Timu ya walemavu yajiandaa kwa michezo ya mpira wa vikapu

Thursday, February 5th, 2009

Timu ya watu walio na ulemavu inajiandaa kwa michezo ya mwaka huu ya mpira wa vikapu itakayofanyika nchini Misri.Mshirikishi wa michezo ya watu walio na ulemavu tawi la North Rift Joseph Ochieng amesema timu hiyo inatarajiwa kuelekea Misri mwishoni mwa mwezi huu.
Ochieng ana imani kuwa timu yake itafanya vyema kufuatia mazoezi kabambe ambayo wachezaji wamefanya.
Hata [...]

Mashindano ya riadha ya wilaya kufanyika wikendi

Thursday, February 5th, 2009

Maandalizi yote ya mashindano ya mbio za riadha za wilaya mkoani bonde la ufa wikendi hii katika uwanja tofauti zimekamilika.Kulingana na duru, wakimbiaji watashiriki katika viwango tofauti zinazojumuisha vijana na wanaume na wanawake wa umri mkubwa katika mbio tofauti.Timu zitakazochaguliwa katika mashindano hayo ya wilaya zitakutana huko Nandi ili kuchaguwa timu itakayoiwakilisha eneo la North [...]